top of page

Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Linaelekea Ukingoni ambapo mwisho wa Mwezi huu wa nane Mshindi mmoja wa shindano hilo la TMT ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali kubwa.
 

 Shindano la TMT ni shindano ambalo limekuwa likiteka hisia za washiriki pamoja na wadau na watazamaji wa kipindi hiko cha TMT ambacho kimejizolea umaarufu nchini na nje ya Nchini kutokana na Umahiri wake ambapo awali shindano hilo lilianza kanda ya ziwa Mkoani Mwanza kwaajili ya kusaka vipaji vya kweli vya kuigiza ambapo baadae safari ilielekea katika kanda nyingine za Tanzania ambapo washindi watatu kutoka kila kanda waliweza Kupatikana na hatimaye kufanya jumla ya washiriki ishirini kutokana kanda sita za Tanzania Kuwasili Jijini Dar Es Salaam, Mwishoni mwa Mwezi wa Sita ambapo waliweka kambi na kuanza kupewa mafunzo na Mwalimu Kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam aitwaye Dk Mona Mwakalinga akisaidia na Mwl Issa.

 

Washiriki Hao 20 waliweza pia kupata fursa ya kufanya filamu fupi ambazo ziliweza kupima uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kutoka darasani na hatimaye kupelekea watazamaji kuweza kuwapigia kura huku wakisaidiana na majaji wa Shindano hilo. Majaji wa shindano hilo ni Roy Sarungi, Vyonne Cherry na SIngle Mtambalike.

 

Mpaka sasa Jumla ya Washiriki 7 wameshatoka kwenye kinyanganyiro na kupelekea kubaki na washiriki wengine 13 ambapo washiriki watatu wanatakiwa kutoka na kubaki washiriki 10 huku kumi hao wakiwa wameingia fainali sasa ya kuzisaka zile Milioni hamsini ambazo Mshindi mmoja atajinyakulia siku ya Fainali inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi wa 8.

 

Ili kuweza kumbakiza mshiriki wako unachotakiwa kufanya ni Kumpigia Kura kwa wingi kupitia Simu yako ya mkononi kwa kuandika Neno "TMT" acha nafasi namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano "TMT" 00 halafu tuma kwenda 15678 au Pia unaweza kumpigia kura mshiriki umpendae kupitia ukurasa wetu wa facebook kwa kutembelea anuani ifuatayo https://www.facebook.com/tztmt.

 

Washiriki Kumi watakaoingia Kwenye Fainali ya Kusaka Milioni 50 watakuwa chini ya Kampuni mahiri ya Utengenezaji na Usamabazaji wa filamu za Kitanzania ya Proin Promotions ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents, Shindano Bora na kubwa Tanzania na la Kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati 

 

Jinsi ya Kumpigia kura Mshiriki umpendae kwa Kutumia Simu ya Mkononi Andika Neno "TMT" ikifuatiwa na namba ya ushiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 tuma kwenda 15678

 

Na Jinsi ya Kumpigia kura mshiriki kupitia ukurasa wetu wa facebook BOFYA HAPA  kwa kupata maelezo.

 

 

Ni jumamosi ya wiki ijayo pale Mlimani City ambapo Ndipo yule mshindi wa TMT atapatikana na kushinda milioni hamsini.....usikoseeeeeeee

Kumpigia kura umpendae - Tuma neno
TMT Kwenda 15678

follow us:

© 2015 by Poseidon, all rights reserved.

  • Facebook Classic
  • Twitter Classic
  • c-youtube
bottom of page